pmbet

Tutakagua mara kwa mara - LATRA

Sisti Herman

December 25, 2023
Share :

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani kwa pamoja wamesema Serikali itaendelea kusimamia Usalama wa Vyombo vya moto hapa nchini na kufanya kaguzi za mara kwa mara na kutoa elimu kwa Madereva kumaliza ajali nchini huku Mamlaka hiyo ikiwataka Mawakala wa Mabasi kuandika taarifa kikamilifu ili kuwapa haki abiria kipindi inapotokea suala la malipo ama ajali.

Hayo yamesemwa Mkatika kituo kikuu cha mabasi Jijini Arusha na Bw. Johansen Kahatano, Mkurugenzi Udhibiti Usafiri wa Barabara kutoka LATRA ambapo amebainisha kuwa wapo katika muendelezo wa ukaguzi wa vyombo vya moto nchini na kufuatilia huduma za usafirishaji ili kubaini changamoto zilizopo na na kuzifanyia kazi kwa wakati.

Ameongeza kuwa katika ukaguzi huo wameangalia nauli zinazolipwa kama ni nauli halali zilizotolewa na Serikali mapema mwezi huu huku akiwapongeza watoa huduma kwa kujipanga vyema kipindi hiki cha mwisho wa mwaka ambapo wanaendelea kutoa huduma nzuri kwa wananchi.

Mkurungenzi huyo pia amesema kuna changamoto ambazo ni uandishi wa taarifa za abiria ambazo ni muhimu katika matumizi ya malipo ya kifedha ambapo amewataka mawakala kurekebisha mara moja changamoto hiyo.

Aidha Bwana Kahatano amesisistiza kuwa mawakala kote nchini wanapaswa kufuata sheria zilizopo huku akiwataka kuandika taarifa kamili za abiria ambazo zipo kwa mujibu wa sheria na taratibu za Mamlaka ya udhibiti usafiri Ardhini LATRA.

Pia amewataka mawakala hao kuandika vyema utambulisho wa mizigo ya abiria ili kuondoa changamoto ya upotevu wa mizigo ya abiria.

Nao baadhi ya abiria wanaotumia vyombo hivyo kwenda maeneo tofauti tofauti ya nchi na nje ya nchi wasema ni vyema abiria wakatekeleza wajibu wao pindi wanaponda magari hayo kufunga mikanda ili iwasadie huku wakitaka Madereva nao kufuata sheria za usalama barabarani zilizopo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet