Tutashinda kwaajili ya mashabiki wetu - Benchikha
Sisti Herman
December 18, 2023
Share :
Kocha mkuu wa Simba Abdelhak Benchikha amesema mchezo wa kesho wa raundi ya 4 ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Wydad AC ni muhimu kwao kwani huamua hatma yao kuvuka hatua ya makundi
“Kesho tuna mechi kubwa dhidi ya Wydad, ni mechi ya muhimu na ya maamuzi kwetu kama ilivyo kwa Wydad, tunapaswa kuwa bora, tunapaswa kuwa makini, natumaini hakuna kinachoweza kuharibu mechi na na imani wachezaji wangu wanajiamini na watulivu, watajituma kushinda kwaajili ya mashabiki wetu” alisema Benchikha kwenye mkutano na waandishi wa habari
Mahojioano ya Benchikha utayapata kwa urefu zaidi kwenye mtandao wa Youtube wa PMTV