pmbet

Tutatoa timu uwanjani ubaguzi ukijirudia leo - Thibaut Courteous

Eric Buyanza

February 25, 2026
Share :

Real Madrid wako tayari kuondoka uwanjani endapo kutakuwa na tukio jingine la ubaguzi dhidi ya wachezaji wao, hasa baada ya Vinicius Junior kukumbana na maneno ya ubaguzi kutoka kwa mchezaji wa Benfica, Gianluca Prestianni, katika mchezo wa kwanza wiki iliyopita.
 

Mlinda mlango wa timu hiyo Thibaut Courteous amesema kuwa itakapo walazimu kutoka uwanjani itabidi iwe hivyo, lakini akisisitiza kuwa Vinicius ndiye atakayekuwa na neno la maamuzi ya mwisho.
 

Prestianni amesimamishwa na UEFA kwa mchezo mmoja, na Real Madrid wameonyesha mshikamano wao na Vinicius, huku kocha wao Alvaro Arbeloa akisema kuwa Vinicius ni "mpiganaji" na atapambana na ubaguzi.
 

Real Madrid wanakipiga na Benfica leo kwenye mchezo utakaochezwa saa 5 usiku.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet