Tutawatoa Simba - Nizar
Sisti Herman
January 9, 2024
Share :
Kocha Msaidizi wa Singida Fountain Gate, Nizar Khalfan amesema mechi ya kesho dhidi ya Simba haitakuwa ya kitoto, lakini ana uhakika wa ushindi kwa maandalizi waliyofanya.
"Hata wao wanajua shughuli yetu, wakikutana na sisi huwa si mechi ya kitoto na wangeambiwa wachague kati yetu na Azam kwenye hatua hii nadhani wangechagua kukutana na Azam na siyo Singida, Kama tukitoka sare dakika 90, basi wao watatoka kwa penati. " - amesema mbele ya wanahabari leo, Nizar
Kuhusu 'utajiri' wa washambuliaji walionao, Nizar amesema haiwapi ugumu benchi la ufundi bali inawarahisishia kazi kwakuwa yeyote anayeanza anatimiza wajibu wake, jambo ambalo ni hamasa kwa wanaoanzia benchi.
Singida Fountain Gate na Simba watacheza kesho saa 2:15 usiku kwenye mchezo wa nusu fainali ya Mapinduzi Cup.