pmbet

Tuwalinde Hersi na makamu wake - Patrick Simon

Eric Buyanza

October 27, 2026
Share :

Mwanasheria wa zamani wa Yanga, Patrick Simon amewataka Mashabiki na Wanachama wa timu hiyo kutoingia katika mtego wa kuwasema viongozi wao wa juu Rais, Hersi Said na Makamu wake Araphat Hajji.

 

“Wananchi wenzangu, msiingie mtego wa kuwasema na kuwakatisha tamaa viongozi wetu, hayo yanayoendelea ni vita nje ya uwanja. Viongozi wetu wanafanya kazi nzuri sana.

 

“Mpaka sasa sisi bado ni Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara na bado tuna nafasi ya kutetea ubingwa wetu. Vile vile, timu yetu imefuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hivo bado tuko ndani ya malengo ya msimu.

 

“Tukaipe support timu yetu ina kazi maalum dhidi ya Mashujaa FC pale KMC Complex, mengine tuwaachie viongozi wetu. Mlindeni Rais wetu na Makamu wake mtanishukuru baadae” ameandika Simon katika ukurasa wake wa Instagram.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet