TV 'yamchomesha' mtoto aliyetoroka shule kwenda kwenye mechi
Sisti Herman
February 4, 2026
Share :

Sammy Scott, shabiki wa Newcastle United mwenye umri wa miaka tisa, alitoroka shule akidai kuwa anaumwa ili kusafiri na baba yake kwenda London kutazama mechi ya nusu fainali ya Kombe la Carabao dhidi ya Arsenal katika Uwanja wa Emirates.
Hata hivyo, siri yake ilifichuka baada ya kamera za televisheni ya Sky Sports kumnasa akishangilia kwa hisia ushindi wa Newcastle wa 2-0. Uongozi wa shule yake uliona picha hizo mubashara na kugundua kuwa mtoto huyo hakuwa mgonjwa kama ilivyodaiwa.
Shule ilichukua hatua ya kuwatafuta wazazi wake ikiwa na ushahidi wa picha (screenshot) iliyopatikana kutoka kwenye matangazo hayo ya TV kumuonyesha Sammy akiwa uwanjani.





