Tv za Cameroon zasita kurusha sehemu za hotuba ya papa
Eric Buyanza
April 16, 2026
Share :

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis XIV amewasili nchini Cameroon na kutoa ujumbe wa kushikilia madaraka kihaki kwa Rais Paul Biya wa nchi hiyo.
Biya ambaye amekuwa madarakani kwa zaidi ya miongominne nchini Cameroon aliongeza muda wake madarakani baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi uliopita uliokumbwa na utata.
Vatican ilikuwa imesema kuwa vita dhidi ya ufisadi katika nchi hiyo ya Afrika ya Kati iliyo na utajiri wa madini ndiyo mojawapo wa ujumbe atakaouwasilisha Baba Mtakatifu.
Kiongozi huyo wa kidini hakusita katika kuwasilisha ujumbe huo kwa Rais Biya na mamlaka nchini humo katika hotuba yake aliyoitoa katika kasri la rais.
Biya aliye na umri wa miaka 93, aliketi kimya huku Papa Leo akisoma hotuba yake kwa Kifaransa.
Televisheni nchini Cameroon zilisita kurusha sehemu za hotuba ya Papa ila haikubainika iwapo ilikuwa ni kwasababu za kiufundi.
DW





