Twiga Stars dimbani kuisaka tiketi ya Olympic 2028
Sisti Herman
October 9, 2026
Share :

Timu ya Taifa ya Tanzania ya wanawake 'Twiga Stars' leo itashuka dimbani kuikabili Botswana katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa raundi ya pili ya kufuzu Michezo ya Olympic Los Angeles 2028.
Mchezo huu utachezwa kuanzia saa 2:00 usiku kwa saa za Tanzania katika Uwanja wa Obed Itan Chilume Stadium.
Hii ni raundi ya pili ya michuano ya kufuzu Olympic, ushindi wa jumla katika michezo miwili utaipeleka timu inayofuzu raundi ya tatu.





