Twiga Stars wafuzu rasmi WAFCON 2024
Eric Buyanza
December 5, 2023
Share :
Timu ya Taifa ya mpira wa miguu wanawake Tanzania "Twiga Stars" imefuzu rasmi Fainali za kombe la mataifa Afrika (WAFCON) zitakazofanyika mwaka 2024 nchini Morocco baada ya kuwaondoa Togo kwa jumla ya mabao 3-2.
Stars walianza kampeni za kuwania kufuzu mashindano hayo mwaka huu kwa kuwaondoa Ivory Coast kwa mikwaju ya penalti baada ya matokeo ya jumla nyumbani na ugenini kuwa sare ya 2-2 kabla ya kuwafurumusha Togo kwenye raundi ya mwisho inayowapa rasmi tiketi ya kuelekea Morocco.
Stars inafuzu Afcon baada ya miaka 13 kwani mara mwisho ilifuzu mwaka 2010 kwenye fainali zilizofanyika nchini Afrika kusini.