Twiga Stars yapoteza mchezo dhidi ya Banyana Banyana kwa 3-0
Eric Buyanza
February 23, 2024
Share :
Timu ya Taifa ya wanawake "Twiga Stars" imepoteza mchezo wa mkondo wa Kwanza wa hatua ya tatu ya mtoano wa kuwania kufuzu michuano ya Olympic 2024 dhidi ya timu ya Taifa Afrika kusini "Banyana Banyana" kwa magoli 3-0 mchezo ulimalizika hivi punde kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Magoli ya Afrika kusini yamefungwa na mshambuliaji wa kati Jermaine Seoposenwe dakika ya 10 na Thembi Kgatlana dakika ya 57 huku Hildah Magaia akitupia msumari wa mwisho kwenye dakika za jioni na kufanya mlima kuwa mrefu kwa Stars.
Tanzania itahitaji ushindi wa magoli zaidi ya mawili ili kuweza kufuzu kwenye mchezo wa mkondo wa pili utakaochezwa nchini Afrika kusini.