Tyla atwaa tuzo yake ya pili ya Grammy 2026.
Joyce Shedrack
February 2, 2026
Share :
Staa wa muziki kutoka Afrika Kusini, Tyla ameshinda tuzo yake ya pili ya Grammy katika kipengele cha Best African Music Performance kwenye Tuzo za Grammy za mwaka 2026.
Ushindi huo umeendelea kuthibitisha nafasi ya Tyla kama mmoja wa wasanii wenye ushawishi mkubwa barani Afrika na duniani kwa ujumla. Kupitia muziki wake, Tyla ameweza kuvuka mipaka ya bara na kuutambulisha muziki wa Afrika katika majukwaa makubwa ya kimataifa.
Tyla ameibuka mshindi mbele ya Davido, Ayra Starr, Wizkid na Eddy Kenzo.





