Tyla awakanyaga vibaya Wanigeria kwenye Tuzo za BET 2024.
Joyce Shedrack
July 1, 2024
Share :
Msanii wa muziki kutoka kwenye ardhi ya Madiba, Afrika Kusini Tyla ameibuka kinara kwenye usiku wa Tuzo za BET 2024 zilizofanyika usiku wa kuamkia leo Los Angeles, Marekani baada ya kunyakua tuzo mbili katika kipengele cha ‘Best International Act’ na kipengele cha Best New Artist.
Msanii huyo amewapiku kwa mara ya pili wasanii kutoka Nigeria kwenye tuzo za kimataifa baada ya kuibuka mshindi kwenye tuzo ya BET 2024 Msanii huyo akiwashinda Ayra Syarr, Asake, Aya Nakamura, Focalistic, BK’, Raye, Cleo Sol na wengine.
Ikumbukwe mwezi Februari mwaka huu Tyla alishinda tuzo yake ya kwanza ya Grammy akiwaburuza wasanii wakubwa kutoka Nigeria akiwemo Burna Boy, Davido, Asake na Ayrra Starr.