Tyson aonyesha picha siku ya kwanza mazoezini, bado anatisha
Eric Buyanza
March 15, 2024
Share :
Wakati tukiendelea kusubiria pambano kubwa la ngumi kati ya mkongwe Mike Tyson na mwanamitindo Jake Paul litakalofanyika Julai 20 katika uwanja maarufu wa AT&T nchini Marekani.
Mkongwe Mike Tyson ameshirikisha mashabiki wa masumbwi picha ya siku yake ya kwanza mazoezini kwa ajili ya kujiandaa na pambano hilo.
Picha hizo za mazoezi zimezua gumzo mitandaoni huku wengi wakionyesha kumuonea huruma Jake Paul kwa kile atakachokuja kukutana nacho, huku wengine wakidiriki kumuonya dogo kuwa bado ana nafasi ya kutafakari mara mbili kabla ya kuingia ulingoni na huyo mzee.