Tyson Fury amtandika Makhmudov, amtaka A.J ulingoni
Sisti Herman
April 11, 2026
Share :

Bondia wa Uingereza Tyson Fury ameshinda mchezo wake wa kwanza baada ya miezi 16 tangu kurejea ulingoni dhidi ya bondia Arslanbek Makhmudov.
'Gypsy King' ameshinda kwa kauli ya pamoja ya majaji wote baada ya kumchakaza vilivyo Arslanbek Makhmudov huku baada ya kutangazwa mshindi akitaja rasmi kuwa pambano lijalo anamtaka Anthony Joshua ambaye pia alikuwa ulingoni.





