pmbet

Tyson Fury na mkewe wanatarajia mtoto wa 8, wanasema "ikifika 10 basi''

Eric Buyanza

April 3, 2024
Share :

Bondia mtata wa nchini Uingereza, Tyson Fury, amedokeza kuwa yeye na mke wake Paris Fury wanatarajia mtoto wa 8.

Wawili hao ni wazazi wa watoto 7 na wamekuwa katika ndoa kwa kipindi cha miaka 15 sasa, na ni miezi sita tu imepita tangu wamkaribishe duniani mtoto wao huyo wa saba.

Kwa mujibu wa Fury, kizazi chake na Paris bado kinaongezeka na mpango wao ni kupanua familia hadi kufikia idadi ya watoto 10.

Siku chache zilizopita bondia huyo alitumia ukurasa wake wa instagram kuielezea picha ya mkewe ambaye sasa ni mjamzito.

“Oneni mke wangu mjamzito alivyo mrembo. Yaani amekwishazaa watoto saba tayari na bado ana nguvu tu! Tutahesabu watoto hadi wafikie 10. Mtoto nambari nane yuko njiani na tunamtarajia duniani hivi karibuni!” aliandika.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet