Uamuzi kesi ya Lissu kutolewa Mei 6
Sisti Herman
April 28, 2025
Share :
Leo April 28,2025 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imesikiliza shauri la Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo taifa (CHADEMA), Tundu Lissu kuhusu kuchapisha taarifa za uongo kwenye mitandao mbalimbali ya Kijamii linalomkabili Tundu Lissu.
Hivyo siku ya leo April 28 Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu ilitarajiwa itoe majibu yaliyowasilishwa na upande wa utetezi kutaka mtuhumiwa (Lissu) awepo mahakamani wakati kesi ikiendelea ambapo baada ya majadiliano, maamuzi ya suala hilo yanatarajiwa kutolewa Mei 6, 2025 ambapo itaamua kama kesi hiyo iendelee kusikilizwa kwa njia ya mtandao au la.
Akizungumza na vyombo vya habari, Mwanasheria wa Chadema Dk. Nshalah Rugemeleza ameeleza kwamba hakimu amesikiliza mapingamizi yao na upande wa Serikali umejibu, na hivyo wanachosubiri ni hukumu hiyo ndogo kutolewa dhidi ya Mwenyekiti Tundu Lissu.