Ubora wa Mukwala na Ahoua utarahisisha kazi ya Fadlu - Hans van der Pluijm
Eric Buyanza
July 27, 2024
Share :
Kocha wa zamani wa Yanga, Hans van der Pluijm amewataja Steven Mukwala na Jean Charles Ahoua kama maingizo mapya katika kikosi cha Simba ambayo yanaweza kurahisisha kazi kwa kocha Fadlu kutokana na ubora ambao ameona kutoka kwao, na amekuwa akivutiwa nao.
“Makocha tumekuwa wafuatiliaji, nipo Ghana lakini huwa nafuatilia ligi za nchi mbalimbali, najua kuwa Simba kwa sasa wanajaribu kukijenga upya kikosi chao, wamefanya usajili mzuri mfano Mukwala amefanya vizuri hapa (Ghana) ni kati ya washambuliaji hatari, namtabiria mazuri,” alisema Hans.
“Ahoua naye amefanya vizuri Ivory Coast, jambo ambalo linaweza kuwa changamoto kwa Fadlu ni moja tu ambalo ni kupata kile kilichobora kwa kila mchezaji, kuwa na wachezaji wazuri ni moja lakini kupata kilichobora kwa wachezaji katika muundo wa timu vile anataka icheze ni jambo jingine, akifaulu hapo huenda Simba ikarejea katika makali yake.”
MWANASPOTI