Uchaguzi Mkuu Afrika kusini, mchuano mkali Ramaphosa, Malema na Zuma
Sisti Herman
May 29, 2024
Share :
Raia wa Afrika Kusini wameanza kupiga kura katika uchaguzi mkuu unaotajwa kuwa muhimu zaidi kwa nchi hiyo ndani ya miaka 30.
Chama tawala cha ANC, ambacho kiliongoza mapambano ya kuondolewa madarakani kwa serikali ya kibaguzi mwaka 1994, kinatabiriwa kushinda uchaguzi huo huku usukani wao ukiwa na Cyril Ramaphosa, Rais wa sasa Taifa hilo licha ya ushindani mkubwa uliopo kutoka kwa wagombea wengine kama Julius Malema (EFF) Jacob Zuma na (uMkhonto we Sizwe).
Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa saa mbili asubuhi na vinategemewa kufungwa saa nne usiku, huku wapigakura milioni 27 walioandikishwa wakichagua bunge jipya litakalo mchagua Rais wa nchi hiyo.