pmbet

Uchaguzi serikali za mitaa utakuwa wa huru na haki - Rais Samia

Eric Buyanza

February 8, 2024
Share :

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema haki, demokrasia, sheria na utawala bora utadumishwa kwa watu wote wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu. 

Rais Samia aliyasema hayo jana katika sherehe za mwaka mpya 2024 (Diplomatic Sherry Party) kwa Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini pamoja na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa zilizofanyika Ikulu. 

Aidha, Rais Samia amesema ili kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki, Kikosi Kazi huru cha kupitia na kushauri mageuzi muhimu katika mfumo wa siasa kiliundwa ambapo kiliwasilisha ripoti yake mwaka 2023. Rais Samia pia amesema mapendekezo mengi ya Kikosi Kazi yaliyopokelewa na serikali na wadau wote yalihusu kuongeza uwazi katika michakato ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na uteuzi wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi. 

Vile vile, Rais Samia amesema masuala machache hayakupokelewa moja kwa moja ambayo yalikuwa kinyume na katiba hivyo yanaweza kuchukuliwa wakati wa mchakato wa marekebisho ya katiba.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet