UCHAGUZI URUSI: Mwanamke achoma moto kibanda cha kupigia kura Moscow
Eric Buyanza
March 16, 2024
Share :
Huko Urusi, mwanamke mmoja amechoma moto kibanda cha kupigia kura katika kituo cha kupigia kura cha Moscow jana Machi 15, 2024, ikiwa ni siku ya kwanza ya uchaguzi wa urais nchini humo.
Hata hivyo shughuli za upigaji kura katika kituo hicho ulirejea baada ya moto huo kuzimwa na mwanamke huyo kukamatwa.
Uchaguzi unafanyika wakati huu Urusi ikiwa kwenye vita na jirani yake Ukraine kwa mwaka wa tatu sasa.
Hata hivyo, wachambuzi wa siasa za Urusi wanasema itakuwa vigumu kumshinda Putin, ambaye amehakikisha wapinzani wake wakuu wamefungwa jela na wengine kukimbia nchi.