Uchebe wa Simba awa kocha Mkuu Singida Black Stars
Sisti Herman
June 7, 2024
Share :
Klabu ya Singida Black Stars (zamani Ihefu Fc) imethibitisha kuingia makubaliano na aliyekuwa kocha wa Simba Sc, kocha Kocha Patrick Aussems raia wa Ubeligiji kuwa Kocha Mkuu klabuni hapo kuanzia msimu mpya wa 2024/25 kwa kandarasi ya awali ya msimu mmoja mpaka tarehe 30 Juni 2025.
Patrick Aussems ni Kocha mwenye leseni ya UEFA PRO na uzoefu wa kufundisha vilabu vikubwa barani Africa, Ulaya na Asia, zikiwemo timu za Al Hilal Omdurman (Sudan), Simba SC (Tanzania), AFC Leaopards (Kenya), Shenzhen Ruby (China), ETG (Evian Thonon STARS Ward) FC & Angers SCO FC France.
Pia ameafundisha timu za taifa mbalimbali zikiwemo za Nepal na Benin. Kocha Aussems amewahi pia kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Marbella FC (Spain).
Kocha Aussems atajiunga na kikosi hicho chenye maskani yake CCM Liti, Singida na kuanza kazi rasmi tarehe 1 Julai 2024. Kwa sasa anaendelea na zoezi la usajili kwa kushirikiana na Menejimenti.