Udeze anaiunga mkono Dr Congo ili wanaigeria wajifunze
Eric Buyanza
March 31, 2026
Share :

Beki wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria Super Eagles, Feanyi Udeze amesema atakuwa sambamba na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inayosaka nafasi ya kucheza Kombe la Dunia la FIFA 2026.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo iliishinda Nigeria katika mechi ya mchujo wa kuwania kufuzu kwa Afrika mwezi Novemba mwaka jana.
Leopards watamenyana na Jamaica kuwania nafasi ya kucheza kombe la Dunia huko Mexico, Canada na Marekani usiku wa kuamkia kesho.
Udeze alifichua sababu ya uamuzi wake wa kuiunga mkono Leopards. "Ninaunga mkono DR Congo kuwa kwenye Kombe la Dunia kwa sababu ninataka wachezaji wa Super Eagles waelewe maana ya kufuzu kwa mashindano makubwa kama Kombe la Dunia, haswa kutokana na kwamba timu iliyokuondoa hatimaye ilitwaa tiketi," Udeze aliiambia Brila FM.





