pmbet

UEFA yaibwatukia FIFA baada ya mchezaji wa Marekani kufutiwa kadi

Eric Buyanza

July 6, 2026
Share :

Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) limeikosoa vikali FIFA kufuatia uamuzi wake wa kutomshughulikia mshambuliaji wa Marekani, Folarin Balogun kwa kusimamisha adhabu yake ya kadi nyekundu aliyopewa kwenye Kombe la Dunia.

 

UEFA imeuita uamuzi huo usioeleweka na usio na msingi, ikieleza kuwa kuingilia utekelezaji wa adhabu wakati mashindano yakiendelea ni kuvuka mipaka ya haki na kanuni za mchezo.
 

Balogun, mwenye umri wa miaka 25, alitolewa kwa kadi nyekundu katika mechi dhidi ya Bosnia jambo ambalo kwa mujibu wa kanuni lilipaswa kumfanya akose mchezo wa hatua ya 16 bora dhidi ya Ubelgiji.
 

Kwa mujibu wa takwimu za Kombe la Dunia, kati ya wachezaji wengine 188 waliopata kadi nyekundu katika historia ya mashindano hayo, ni mchezaji mmoja tu aliyewahi kuepuka adhabu ya kusimamishwa kucheza.

 

Kwa mujibu wa CBS News, uamuzi wa kumruhusu Balogun kurejea uwanjani ulifuatia mazungumzo ya simu yaliyofanyika Alhamisi kati ya Rais wa Marekani, Donald Trump, na Rais wa FIFA, Gianni Infantino, ambapo suala la adhabu hiyo lilijadiliwa.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet