UEFA yaitisha kikao cha dharura kuikabili FIFA
Eric Buyanza
July 30, 2026
Share :

Shirikisho la Soka barani Ulaya (UEFA) limeitisha kikao cha dharura cha wanachama wake wote 55 ili kujadili na kupanga mapambano dhidi ya mpango mpya wa shirikisho la soka duniani (FIFA). Kikao hicho kinafanyika baada ya kuibuka kwa mzozo mkubwa wa kifedha na kiuongozi kati ya taasisi hizo mbili.
Mzozo huu umesababishwa na hatua ya Rais wa FIFA, Gianni Infantino, kutaka kuuza hisa za mashindano makubwa (ikiwemo Kombe la Dunia) kwa wawekezaji binafsi kupitia kampuni mpya itakayofahamika kama FIFA Forward Enterprise (FFE) kwa thamani ya dola bilioni 20.
FIFA imetoa masharti kwa mashirikisho yote wanachama hadi Septemba 19 kukubali mpango huo ili yapewe mgao wa papo hapo wa dola milioni 20 kila mmoja, vinginevyo yatakosa bonasi hiyo. UEFA inaona kitendo hiki ni kama FIFA inataka "kujitajirisha yenyewe na marafiki zake"....huku ikisema kuwa mpira sio mali binafsi ya FIFA ya kuweza kuiuza kwa wawekezaji binafsi.
Mpango huo ulitangazwa kupitia vyombo vya habari bila UEFA au vilabu vikuu vya Ulaya kushirikishwa mapema.





