Ufaransa kuruhusu wenye magonjwa yasiyotibika kujiua
Eric Buyanza
July 17, 2026
Share :

Bunge la Ufaransa limepiga kura na kupitisha mswada wa sheria unaoruhusu watu wazima wenye magonjwa yasiyotibika na yanayohatarisha maisha kuomba kusaidiwa kufa (assisted dying).
Muswada huo ulipitishwa Jumatano jioni kwa kura 291, lakini haujawa sheria rasmi kwa maana utahitaji mapitio ili kubaini ikiwa haukiuki Katiba ya Ufaransa. Muswada huo uliowasilishwa na utawala wa Rais Emmanuel Macron, uliibua mjadala bungeni kwa takriban miaka mitatu hasa kuhusu huduma hiyo ya kimatitabu ya kusitisha maisha ya mgonjwa aliyekata tamaa.
Kulingana na makadirio mbalimbali, watu milioni 300 duniani kote huomba huduma hii inayofahamika kwa kiingereza kama "Euthanasia" ambayo huruhusiwa kwa kuzingatia masharti kadhaa. Mataifa kadhaa ya Ulaya ikiwa ni pamoja na Ubelgiji na Uholanzi yanaruhusu huduma hii ya kufupisha maisha kwa watu wenye magonjwa yasiyopona na wanaoteseka kupita kiasi.





