pmbet

Ufaransa yapitisha muswada unaowapa wanawake haki ya kutoa mimba

Eric Buyanza

February 29, 2024
Share :

Baraza la Seneti la Ufaransa limeidhinisha muswada wa sheria wa kuweka katika katiba ya nchi haki ya mwanamke kutoa mimba.
 

Muswada huo sasa utawasilishwa mbele ya kikao cha bunge ili uidhinishwe na theluthi tano za wabunge wiki ijayo.
 

Macron alisema baada ya kura hiyo kwamba serikali yake ina dhamira ya kufanya haki ya utoaji wa mimba kwa wanawake iwekwe bila kipingamizi katika katiba ya nchi.
 

Baraza la Seneti lilipitisha muswada huo kwa kura 267 dhidi ya 50. Waziri wa sheria Eric Dupond-Moretti alisema “Kura hii ni ya kihistoria,” akiongeza kuwa Baraza la Seneti limeandika ukurasa mpya katika haki za wanawake.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet