pmbet

Ufaransa yasema Iran itapigwa ikikataa mazungumzo ya nyuklia

Eric Buyanza

April 3, 2025
Share :

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa alionya jana Jumatano kwamba njia ya kuikabili Iran kijeshi haitaepukika ikiwa mazungumzo juu ya mpango wa nyuklia hayatafanikiwa. 

"Kipaumbele chetu ni kufikia makubaliano ambayo kwa hakika na kwa uthabiti yanazuia mpango wa nyuklia wa Iran," 

Jean-Noel Barrot aliwaambia wabunge. 
"Ikitokea kushindwa, makabiliano ya kijeshi hayataepukika na yatavuruga sana eneo hilo.” Barrot alisema.

“Ujasiri wetu na imani yetu inabaki kuwa sawa, Iran haipaswi kamwe kupata silaha za nyuklia.”

Rais wa Marekani Donald Trump ametishia kuwa Iran itashambuliwa kwa mabomu iwapo itaendelea kutengeneza silaha za nyuklia. 

Kiongozi mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, ameahidi kulipiza kisasi ikiwa atashambuliwa na marekani au washirika wake.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet