Uganda inataka raia washtakiwe kwenye mahakama za kijeshi
Eric Buyanza
April 19, 2025
Share :
Serikali ya Uganda, inapanga kuwasilisha muswada bungeni, ili kupitisha sheria itakayoruhusu raia wa kawaida, kushtakiwa katika Mahakama za kijeshi.
Waziri wa Sheria, Nobert Mao, amesema muswada huo uko tayari, na sasa unasubiri kupitishwa na Baraza la Mawaziri, kabla ya kuwasilishwa bungeni.
Mao amesema, muswada huo, umeeleza baadhi ya mashtaka ambayo, raia wa kawaida anaweza akashtakiwa kwenye Mahakama za kijeshi.
Hatua hii imezua mjadala mkubwa nchini Uganda.