pmbet

Uganda tuko tayari kuisaidia Israel wakituomba msaada - Jenerali Muhoozi

Eric Buyanza

March 27, 2026
Share :

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba,ambaye pia ni mtoto wa Rais Yoweri Museveni ametangaza kwamba Uganda itaiunga mkono Israel ikiwa taifa hilo litahitaji msaada.

 

Katika mfululizo wa jumbe zake kwenye mtandao wa X, Muhoozi alisisitiza Uganda iko tayari kutoa msaada wa kijeshi ikiwa utahitajika

 

Kauli zake zinakuja wakati mvutano ukiongezeka kati ya Iran, Marekani na Israel, huku wasiwasi wa kimataifa ukiongezeka baada ya kufungwa kwa Mlango wa Hormuz kuvuruga njia muhimu za biashara.
 

“Tunahitaji vita vya Mashariki ya Kati vikome sasa. Dunia imechoshwa navyo. Lakini mazungumzo yoyote ya kuiharibu au kuishinda Israel yatatuingiza vitani. Upande wa Israel!” aliandika.
 

Kainerugaba alienda mbali zaidi, akisema kwamba Uganda iko tayari kutoa msaada wa moja kwa moja wa kijeshi ikiwa utaombwa na Waisraeli. “Ikiwa Israel inahitaji msaada, inachotakiwa ni kuomba tu. Ndugu zao wa Uganda wako tayari kusaidia,” aliongeza.
 

“Ikiwa Tehran itathubutu kutupiga kwa makombora. Tutalipiza kwa makombora yetu wenyewe,” akatamba Jenerali Muhoozi.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet