pmbet

Uganda yapitisha sheria ya kuzuia wageni kuingilia mambo yao

Eric Buyanza

May 6, 2026
Share :

Bunge la Uganda limepiga kura kupitisha sheria tata ambayo Kampala inasema inalenga kukabiliana na wageni wanaoingilia masuala yake ya ndani.
 

Sheria hiyo ambayo pia inatumika nchini Urusi na China, imepitishwa licha ya wanaharakati wa haki za kibinadamu, wanahabari na wafanyibiashara kuipinga.

Wakosoaji wa sheria hiyo wanaona kuwa imepitishwa kuwakabili wapinzani wa Rais Yoweri Museveni, aliyetawala taifa hilo kwa mkono wa chuma kwa karibu miongo minne.
 

Kwa mujibu wa Serikali, Sheria hiyo inalenga kulinda maslahi ya nchi dhidi ya wale iliyowataja kuwa ‘mawakala wa mabeberu’, ambao inadai wamekuwa wakitumika kujaribu kutatiza utangamano na usalama wa nchi hiyo.

 

Chini ya sheria hii watu wanaopokea msaada kutoka kwa wafadhili wa kigeni kwa sasa watachukuliwa kama maajenti wa mataifa ya kigeni, ambapo ukipatikana na hatia utakabiliwa na kifungo cha miaka 20 jela.

 

Kufuatia mjadala mkali bungeni, sheria hiyo ilifanyiwa marekekebisho kadhaa ikiwemo kuondoa kipengele kilichowataja raia wake walioko nje kama mawakala wa kigeni na pia kutoziwajibisha taasisi zitakazokaguliwa na Serikali ikiwa zitapokea msaada kutoka nje.

 

Rais Museveni ambaye alichaguliwa mwezi Januari mwaka huu kwa muhula mwingine, amekuwa akizikosoa baadhi ya asasi za kiraia na baadhi ya raia anaodai zimekuwa zikitumika vibaya na mataifa yan je ikiwemo kuhamasisha ushoga.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet