Uganda yawaita wachezaji wa Ughaibuni wenye asili ya nchi yao kwaajili ya AFCON 2027
Sisti Herman
September 28, 2026
Share :

Kuelekea Katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027) shirikisho la mpira Uganda kwa kushirikiana na Serikali ya Taifa hilo imefanikisha kuwarejesha wachezaji wenye asili la taifa hilo kutumikia timu ya taifa ya Uganda katika kampeni za kufuzu katika mashindano ya AFCON 2027 wakiwa na lengo kuu la kuwatumia katika mashindano hayo.
Wachezaji waliojumuishwa, wametoka ligi za Belgium, Malta, Poland, Switzerland, USA, England, Austria na Sweden ambao ni pamoja na Noble Okello, Nathan Asiimwe, Abdoulaye Sissako, Akpan David Udoh na Kelvin Owusu Boateng.
Serikali ya Uganda imelichangia shirikisho kiasi cha shilling za kitanzania billion 1 ( 1.5 billion ugx) katika kampeni hiyo ya kuwarejesha wachezaji wenye asili ya Uganda ambapo mpaka sasa wamefanikiwa kuwatambua wachezaji 200 , Ambao kati ya hao 20 wamevutiwa nao na kuwafatilia kwa kina na kati ya hao 20 tayari wachezaji 9 wameitwa kujiunga na timu ya taifa ambayo ipo kambini hivi sada ikijiandaa na michezo ya kufuzu AFCON.





