Uholanzi kuipatia Ukraine Patriot kwa ajili ya kujilinda
Eric Buyanza
June 22, 2024
Share :
Waziri wa Ulinzi wa Uholanzi Kajsa Ollongren ametangaza jana kwamba taifa hilo pamoja na nchi nyingine wataipatia Ukraine mfumo wa ziada wa ulinzi wa angani wa Patriot, limesema shirika la habari la Uholanzi ANP.
Ollongren amesema Uholanzi itatoa mfumo wa pili wa Patriot kwa Kiev wiki hii, baada ya kukabidhiwa mfumo mwingine na Romania.
Ollongren pia aliwaomba washirika wengine wa Umoja wa Ulaya kutoa vifaa zaidi vya kujilinda kwa Ukraine.