Uholanzi kutoa makombora laki 8 kwa ukraine, ili kupambana na urusi
Eric Buyanza
March 2, 2024
Share :
Waziri Mkuu wa Uholanzi Mark Rutte amesaini mkataba wa ulinzi na Ukraine katika mji wa kaskazini mashariki wa nchi hiyo wa Kharkiv.
Rutte alisema Uholanzi itasaidia kufadhili makombora laki nane kwa ajili ya kuzuia mashambulizi ya majeshi ya Urusi.
Rutte alikutana na Rais Zelenskiy katika ziara ya kushtukiza huko Kharkiv na amekuwa kiongozi wa saba wa nchi za Magharibi kusaini mkataba wa usalama wa miaka kumi na Ukraine katika kipindi cha miezi miwili iliyopita.
Ukraine ina upungufu mkubwa wa silaha wakati ambapo majeshi yake yanajaribu kuwazuia majeshi ya Urusi amba wanafanya mashambulizi kwa mara nyengine mashariki mwa nchi hiyo, miaka miwili baada ya uvamizi kamili ya Urusi ulipoanza.