Uhuru Kenyatta achagua upande Nasimama na Wakenya.
Eric Buyanza
June 26, 2024
Share :
Rais Mstaafu wa Kenya, Uhuru Kenyetta ameutaka uongozi uliopo madarakani ukiongozwa na Raisi William Ruto kuwasikiliza wananchi ili kurejesha amani Nchini humo kufuatia maandamano yanayoendela ya kupinga Muswada wa Fedha 2024.
Kupitia barua aliyoitoa Rais huyo mstaafu amesema Viongozi wanapaswa kutambua kuwa madaraka na mamlaka waliyonayo wamepewa na Wananchi hivyo kuwasikiliza Watu ni lazima na sio jambo la hiari.
“Wapendwa Wakenya nasimama nanyi na naomba Uongozi uzungumze na Wananchi, naomba amani na maelewano kwa kila Mkenya na sote tukumbuke Kenya ni kubwa zaidi kuliko mmoja wetu” -Kenyatta
Kenyatta amesema uongozi unatakiwa kuchukua uamuzi sahihi wa kusikiliza na kutowapuuza watu kwa sababu vurugu kwa pande zote mbili sio suluhisho la matatizo .