Uhusiano na msanii mwenzangu NO, Cha kufa na presha kitu gani? - Maua Sama
Eric Buyanza
July 1, 2024
Share :
Linapokuja swala la mapenzi kila mmoja anakuwa na misimamo yake, kwa upande wa
Msanii wa Bongo Fleva, Maua Sama, yeye anasema hana mpango wala hatarajii kijiingiza kwenye uhusiano wa kimapenzi na msanii mwenzake kwasababu hataki kufa kwa presha.
“Ukiwa na uhusiano na msanii, jiandae kupata presha au kufa kabisa, ndio maana siwezi kabisa kuwa na uhusiano na msanii kwa sababu anaweza akafanya video na mdada mwenye sifa zote ukiangalia sura anayo, shepu ndio usiseme, cha kufa na presha ni kitu gani? Wala siwataki,” amesema.
NMG