pmbet

Ujenzi wa uwanja wa AFCON 2027 Zanzibar wafikia 80%

Sisti Herman

August 19, 2026
Share :

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi, amesema kuwa Uwanja wa AFCON unaojengwa Fumba utakuwa ni kituo cha kisasa chenye viwango vya kimataifa na kichocheo cha kufungua fursa mbalimbali kwa wananchi wa Zanzibar.

 

Dkt. Mwinyi aliyasema hayo leo, tarehe 18 Agosti 2026, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa Uwanja wa AFCON na Bandari ya Fumba katika Mkoa wa Mjini Magharibi.

 

Alisema kukamilika kwa uwanja huo kutaiwezesha Zanzibar kunufaika na fursa za biashara, huduma za ukarimu na fursa nyingine za kiuchumi zitokanazo na ongezeko la wageni, hasa wakati wa mashindano ya AFCON ya mwaka 2027.

 

Rais Mwinyi alisema Serikali itaendelea kuhakikisha kuwa miundombinu inayozunguka uwanja huo inajengwa kwa ubora wa juu na viwango vinavyokubalika kimataifa, ili kuongeza thamani ya eneo hilo na kuleta manufaa ya muda mrefu kwa Zanzibar.

 

Kwa sasa, ujenzi wa Uwanja wa AFCON wa Fumba umekamilika kwa takriban asilimia 80, huku kazi ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali saidizi ikiendelea, ikiwemo barabara ya kisasa inayolenga kuboresha usafiri na kuongeza mvuto wa eneo hilo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet