pmbet

Ujerumani wajiandaa kuipa Ukraine kombora hatari la Taurus

Eric Buyanza

May 27, 2025
Share :

Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz jana Jumatatu ametangaza kwamba Ujerumani, pamoja na Ufaransa, Uingereza na Marekani, zimeondoa vikwazo vyote dhidi ya silaha wanazotuma Ukraine kuisaidia katika vita dhidi ya Urusi.

Kwa kauli hiyo ni kama inatoa kibali kwa Ukraine cha kumtandika Urusi kwa kutumia silaha zote anazopewa bila masharti yoyote kutoka kwa nchi hizo.

"Hakuna tena vikwazo vyovyote vya silaha zinazowasilishwa Ukraine - sio kwa Uingereza, Ufaransa, Ujerumani wala Wamarekani," alisema Merz akiwa mjini Berlin.

"Hii ina maana kwamba Ukraine sasa inaweza kujilinda, kwa mfano, kwa kushambulia kambi za kijeshi za Urusi" Merz alisema.

Wakati hayo yakiendelea kuna taarifa kwamba Ujerumani inajiandaa kuipatia Ukraine makombora hatari ya Taurus. 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet