pmbet

Ujerumani yahalalisha bangi, yaruhusu watu kulima majumbani

Eric Buyanza

April 2, 2024
Share :

Ujerumani imehalalisha bangi kwa matumizi ya burudani licha ya pingamizi kali kutoka kwa wanasiasa na wanaharakati wa masuala ya afya wanaosema hatua hiyo itaongeza matumizi yake miongoni mwa vijana.
 

Hatua hiyo ina maana kwamba watu wenye umri wa zaidi ya miaka 18 sasa wanaruhusiwa kubeba gramu 25 za bangi na kulima hadi mimea mitatu ya bangi katika makazi yao.
 

Kwa maana nyingine inamaanisha kuwa bangi sio marufuku tena nchini Ujeremani na hii ni habari njema kwa watumiaji wanaokadiriwa kufikia Milioni 4.5.
 

Wizara ya afya inasema hatua hii itasaidia kuzuia masoko yasiyo rasmi yanayouzwa bangi, yanayozalisha Euro Bilioni 4 kila mwaka.
 

Kuanzia Julai mosi, watu wazima wataruhusiwa kununua bangi kutoka kwenye vilabu maalum, ambapo kila mmoja atapata hadi gramu hamsini za bangi kila mwezi.
 

Hata hivyo wanaharakati wa afya wanapinga hatua hiyo kwa msingi kuwa matumizi ya bangi miongoni mwa vijana yataathiri mfumo wa maisha kwa watumiaji.
RFI

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet