Ujue utamaduni huu wa kumtemea mate Bibi harusi
Eric Buyanza
July 1, 2024
Share :
Miongoni mwa makabila ya Wamasai wa Tanzania na Kenya, wamekuwa wakiuenzi utamaduni flani wa kipekee tangu enzi na enzi.
Utamaduni huo unaojulikana zaidi kama sherehe ya 'Kutema mate', ni tambiko linalofanywa na Baba ya Bibi harusi kabla binti hajaondoka nyumbani.
Utamaduni huu unaweza kuonekana wa ajabu kwa wengine lakini kwa wamasai una maana kubwa.
Wakati wa sherehe hii, Baba hutemea mate kichwa na kifua cha binti yake, muda mfupi kabla ya harusi ikiwa ni ishara ya kumpa baraka, hekima na bahati nzuri huko aendako (kwa mume).
Ni njia ya Baba kumtakia bintiye ndoa yenye furaha na mafanikio.