Ukata! Barcelona yataka kumuuza Raphina, mwenyewe hataki kuondoka
Eric Buyanza
April 1, 2024
Share :
Klabu ya Barcelona ya Uhispania iko tayari kupokea ofa kwa ajili ya kumuuza mchezaji wake Raphinha msimu huu wa joto ili kupunguza ukata wa kifedha unaoikabili klabu hiyo ya Catalunya.
Hata hivyo mshambuliaji huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 27 hataki kuondoka klabuni hapo.