pmbet

Ukikutwa na silaha haramu faini Milioni 15 au kifungo cha miaka 10.

Joyce Shedrack

October 5, 2026
Share :

Wananchi wametakiwa kusalimisha kwa hiari silaha na risasi wanazomiliki bila vibali, huku zikiwa zimesalia siku 27 kabla ya kumalizika kwa kipindi cha msamaha kilichotolewa na Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Tanzania.

 

Msamaha huo umetolewa kwa mujibu wa Kifungu cha 66 cha Sheria ya Udhibiti wa Silaha na Risasi, Sura ya 223, Marejeo ya Mwaka 2023.

 

Akizungumza leo Oktoba 5, 2026, katika Vijiji vya Mafisa, Majengo, Kibilashi na Stand Kubwa, Wilaya ya Kilindi, Mkoa wa Tanga, Mkuu wa Dawati la Elimu na Udhibiti wa Silaha kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Kamisheni ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Kitengo cha Silaha, 

 

Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Sebastian Madembwe, amesema bado kuna baadhi ya wananchi wanaomiliki silaha bila vibali halali.

ACP Madembwe amewataka wananchi hao kuzisalimisha mara moja kwa hiari ili kunufaika na kipindi cha msamaha kinachotolewa na Serikali.

 

Amesema baada ya kumalizika kwa kipindi hicho, Jeshi la Polisi litaanza misako katika maeneo mbalimbali nchini dhidi ya watu watakaobainika kumiliki silaha kinyume cha sheria, na watakaokamatwa watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

 

Kwa mujibu wa sheria, mtu atakayebainika kumiliki silaha kinyume cha sheria anaweza kuhukumiwa kifungo cha hadi miaka 10, faini ya shilingi milioni 15 au adhabu zote kwa pamoja.

 

Kampeni ya usalimishaji wa hiari wa silaha na risasi ilianza rasmi Septemba 1, 2026, na inatarajiwa kuhitimishwa Oktoba 31, 2026.

Kampeni  hiyo ilizinduliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Paschal Patrobas Katambi, kwa lengo la kuwahamasisha wananchi wenye silaha na risasi wanazomiliki bila vibali kuzisalimisha kabla ya kumalizika kwa kipindi cha msamaha.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet