pmbet

Ukikutwa unamiliki silaha ya marehemu jela miaka 15

Eric Buyanza

June 28, 2024
Share :

Jeshi la Polisi limewataka Wananchi kusalimisha silaha zilizokuwa zinamilikiwa kihalali na ndugu zao ambao kwa sasa ni marehemu, ili silaha hizo zisilete madhara katika jamii na kusema kuendelea kuhifadhi silaha hizo nyumbani ni kinyume cha sheria na atakayepatikana akimiliki silaha hizo akikutwa na hatia Mahakamani anaweza kufungwa miaka 15 jela au faini ya shilioni milioni 10 au vyote kwa pamoja.
 

Taarifa hiyo imetolewa leo Juni 28, 2024 na Msemaji wa Polisi, David Misime.

“Kwa mujibu wa kifungu cha 55 cha Sheria ya Udhibiti wa Silaha na Risasi ya Mwaka 2015 ni kwamba mmiliki wa silaha mara anapofariki, ndugu wa marehemu wanapaswa kuisalimisha silaha hiyo katika kituo cha Polisi kilicho karibu wakati taratibu za mirathi na umilikishwaji kwa mtu mwingine kwa mujibu wa sheria zikiendelea”
 
“Watambue kuwa kuendelea kuhifadhi silaha hizo nyumbani ni kinyume cha sheria na yeyote atakayepatikana akimiliki silaha hizo atakuwa ametenda kosa na endapo akipatikana na hatia Mahakamani, anaweza akapewa adhabu ya kutumikia kifungo cha miaka kumi na tano jela au faini ya shilingi milioni kumi au vyote kwa pamoja”

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet