"Ukimdhuru Mmarekani, tutajibu" - Joe Biden
Eric Buyanza
February 3, 2024
Share :
Rais wa Marekani Joe Biden ametoa taarifa kuhusu mashambulizi ya kulipiza kisasi.
"Leo kwa maelekezo yangu, vikosi vya kijeshi vya Marekani vilishambulia vituo vya Iraq na Syria ambavyo Jeshi la Ulinzi la Iran la Revolutionary Guards Corps (IRGC) na wanamgambo washirika hutumia kushambulia vikosi vya Marekani," alisema.
"Hatua yetu imeanza leo. Jibizo hili litaendelea katika nyakati na maeneo tunayochagua."
Biden alisema Marekani "haitafuti mzozo katika Mashariki ya Kati au popote pengine duniani" lakini alitoa onyo.
"Wacha wale wote ambao wanatafuta kutudhuru wajue hili: Ukimdhuru Mmarekani, tutajibu."