Ukimtaka Davido kwa show, uwe na Bilioni 1.5!
Eric Buyanza
January 6, 2024
Share :
Mwanamuziki wa muziki wa Afrobeat kutoka Nigeria, Davido amewaacha wengi wakitafakari bila kupata majibu baada ya kuweka wazi kiasi anachotoza kutumbuiza kwenye shoo yake moja.
Davido anasema sasa anatoza $600,000 kwa shoo moja (sawa na shilingi bilioni 1 na laki 5 za Tanzania).
"Yaani sasa natoza $600,000 kwa ajili ya show na nafanya shoo tatu hadi nne kwa mwezi, ambazo ni dola milioni 2 hadi 3,” alisema.