"Ukiona hujaelewa hotuba yake basi jua haikuhusu"Ahmed Ally.
Joyce Shedrack
July 15, 2025
Share :
Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ally ameandika ujumbe kuhusu hotuba aliyoitoa usiku wa jana Rais wa heshima wa klabu hiyo Mohamed Dewji.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ahmed Ally ameandika ujumbe ufuatao.
"Hotuba ya Rais wetu @moodewji aliyoitoa jana ni moja kati ya hotuba bora sana ambayo inatoa taswira chanya ya maendeleo ya klabu yetu
Hotuba yake imejikita katika maeneo matatu, Simba ilipotoka, Ilipo na tunapoelekea
"Nimevutuwa zaidi na TUNAPOELEKEA na natamani kila Mwana Simba ajikite kwenye kuitazama mbele yetu"
"Mo ameanisha point 9 ambazo zinaonesha mwelekeo mzuri wa klabu yetu.
1. Kwa mshikamano wetu msimu ujao tunarudi kwa nguvu zaidi
2. Ndoto yangu ni kuiona Simba inakua Ubingwa wa Afrika
3. Tuachane na fitina zisizo na misingi tujenge palipotoboka, tuzibe ufa panapovuja na tusonge mbele bila kuoeneshana vidole
4. Msimu ujao tunarejea kwa nguvu mpya kipaumbele chetu kikubwa ni kufanya usajili makini utakaongeza ushindani
5. Tutaongeza nguvu ya Benchi la ufundi ili kuhakikisha timu yetu inapata muongozo sahihi na kufikia mafanikio
6. Tutaimarisha bodi ya Wakurugenzi
7. Nimetenga fedha za kutosha kuhakikisha timu yetu inakua bora zaidi
8. Tusimame pamoja tuendelee kushirikiana na kulinda heshima ya klabu yetu
9. Sitaacha kuipigania Simba
"Kwenye Points hizi 9 zipo ambazo zinamhusu Mo peke yake lakini zipo ambazo zinatuhusu Wana Simba wote
Zile ambazo zinatuhusu wote hatuna budi kuzimamia ipasavyo ili timu yetu iweze kupiga hatua kwenda mbele
Ukiona hujaelewa hotuba yake basi jua haikuhusu"Ameandika Ahmed Ally.