pmbet

Ukiwa na 'Akili finyu', ndio utaamini napata hela kwenye muziki tu - Lukamba

Eric Buyanza

April 3, 2024
Share :

Aliyewahi kuwa mpiga picha wa Diamond Platinumz, Lukamba amefunguka na kusema ni wale wenye akili finyu tu ndio watakaodhani kuwa yeye anapata hela au anategemea kupata hela kupitia muziki tu.
 

Lukamba ambaye kwasasa pia muongozaji wa filamu anasema kuna vitu vingi sana anafanya kwenye maisha ukiachilia muziki ikiwemo biashara na mambo mengine mengi ili kumuingizia kipato.
 

"Ukiwa unataka kufanya kitu kikubwa halafu unategemea tu muziki....muziki pekee yake hautoshi , hautoshi kuweza kumaintain kufanya filamu kubwa...ndio maana kuna masponsor wanainvest. Lazima kuna namna ushirikiane na watu ili tuweze kutengeneza kitu kikubwa ...mimi peke yangu siwezi kufanya kitu kikubwa na hata mkampuni ya nje yako hivyo...kama unafuatilia makampuni makubwa ya filamu yote yanakuwa yameshirikiana"
 

Lukamba pia amesema anaona sasa ni muda muafaka kwa mashabiki zake kupata kazi nzuri.

 

Fuatilia mahojiano yake kwa urefu kwenye video hapo chini;

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet