"Ukiwa na mtaji wa Milioni 125, serikali inakutambua kama mwekezaji"
Eric Buyanza
January 6, 2024
Share :
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Gilead Terry, amesema kupitia Sheria mpya ya uwekezaji ya 2022, Serikali ya awamu ya sita imeamua kushusha kiwango kinachoweza kutumika kumtambua Mtanzania kama mwekezaji."
Amesema awali Mtanzania alitakiwa kuwa na mtaji wa Takribani Milioni 250 aweze kutambulika kama mwekezaji, sasa hivi kiwango kimeshushwa mpaka takribani Milioni 125. Hivyo Mtanzania yoyote mwenye mzunguko wa biashara wa kiwango hicho anaweza kutambulika kama muwekezaji na akanufaika na mambo mengi.
"Mtaji huu wa Milioni 125 sio fedha peke yake ila ardhi, mali, au mzunguko wa biashara unaofikia kiwango hicho.Kwa upande wa TIC mwaka 2024 ni mwaka wa Uwekezaji tunakwenda na lengo la kuhakikisha mtanzania asiache kutekeleza mradi wake sasa," amesema Gilead Terry