Ukraine inahitaji makombora ya Patriot kujilinda - Trump
Eric Buyanza
July 5, 2025
Share :
Rais wa Marekani Donald Trump amesema Ukraine itahitaji makombora ya Patriot kwa ajili ya ulinzi wake, baada ya kuzungumza na Rais Volodymyr Zelensky siku ya Ijumaa, na kueleza kukatishwa tamaa na Rais wa Urusi Vladimir Putin kushindwa kusitisha mapigano.
Trump aliwaambia waandishi wa habari ndani ya ndege yake ya Air Force One kwamba alifanya mazungumzo ya simu na Zelensky, akirudia kwamba "hakufurahishwa" na mazungumzo ya simu na Putin siku moja kabla, kutokana na kile alichokiita kukataa kwa kiongozi huyo wa Urusi kusitisha mapigano.
Alipoulizwa kama Marekani itakubali kusambaza makombora zaidi ya Patriot kwa Ukraine, kama alivyoombwa na Zelensky, Trump alisema: "Watayahitaji kwa ulinzi... Watahitaji kitu kwa sababu wanashambuliwa sana."