Ukraine washerehekea Krismasi tarehe 25 kwa mara ya kwanza
Eric Buyanza
December 26, 2023
Share :
Wakristo wa Kanisa la Orthodoksi nchini Ukraine jana tarehe 25 Dec kwa mara ya kwanza walisherehekea Krismasi.
Awali, Ukraine walikuwa wakitumia kalenda ya jadi ya ‘Julian’, ambayo pia hutumiwa na Urusi, ambayo kwao krismasi husherehekewa Januari 07.
Matumizi ya kalenda ya ‘Gregorian’ kama yalivyo mataifa mengi ya Magharibi ni muendelezo wa kuchukua hatua za kukinzana na taifa la Urusi.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alibadilisha sheria hiyo mwezi Julai, iliyowaruhusu raia wa Ukraine “kuachana na urithi wa Urusi” ikiwemo kusherehekea Krismasi mwezi Januari.
Katika ujumbe wa Krismasi uliotolewa Jumapili jioni, Zelensky amesema Waukraine wote sasa wapo pamoja.
“Sote tunasherehekea Krismasi pamoja. Katika tarehe hiyo hiyo, kama familia moja kubwa, kama taifa moja, kama nchi moja iliyoungana.” Amesema Zelensky