Ukraine yadungua makombora 12 kati ya 16 ya Urusi na droni 13
Eric Buyanza
June 22, 2024
Share :
Jeshi la Ukraine limedungua makombora 12 kati ya 16 ya Urusi na ndege zote 13 zisizo na rubani usiku wa kuamkia leo Juni 22 huku watu wawili walijeruhiwa.
Hayo yamethibitishwa na Kamanda wa Jeshi la Anga la Kikosi cha Wanajeshi wa Ukraine Nikolai Oleshchuk.
Nikolai amesema katika shambulizi hilo katika mikoa tofauti ya Ukraine, Urusi ilitumia makombora 10 ya (Kh-101/Kh-555) ambapo 7 kati yake yalidunguliwa, na makombora mawili ya Iskander-K (moja llilidunguliwa ) huku makombora 4 ya Caliber. (kila moja likiangushwa).
Kutokana na shambulio hilo la usiku, miundombinu ya nishati iliharibiwa mashariki, magharibi na kusini mwa nchi hiyo, Wizara ya Nishati iliripoti.
BBC